Jumapili 7 Septemba 2025 - 11:30
Maulidi ya kinamama yafanyika nchini Tanzania

Hawza/ Jumuiya ya Shiya Ithnaasharia Tanzania (TIC) ikishirikiana na Hawza ya Imaam Sw'adiq (as), ambayo makazi yake makuu yapo Kigogo Post jijini Daresalam, jana iliadhimisha hafla kubwa ya maulidi ya kinamama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika hali ambayo watu wengi hawakuitarajia wakinamama wa kishia nchini Tanzania wameonekana wakiwa na muamko wa kipekee kabisa baada ya kuanzisha mfumo wa kuadhimisha masiku ya kuzaliwa mtukufu wa daraja Mtume Muhammad (saw), kwa kawaida shughuli kama hizi zimechukua umaaru zaidi zikiwa katika suru ya kuongozwa na jamii ya kiume, lakini kwa wanaharakati na wafuasi wa Ahlulbayt nchini Tanzania imekuwa ni tofauti, kwani kinamama nao pia hawajaachwa nyuma katika shughuli kama hizo.

Siku ya jana sawa na tarehe 7/9/ 2025 wakinamama wa kishia jijini Daresalam walijumuika kwa pamoja katika makao makuu ya Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), ambayo pia ndipo ilipo Markaz ya Hawza ya Im'am Sw'adiq (as), Mjumuiko huo haukuwa na lengo lengine isipokuwa ni kumuenzi Mtukufu wa Daraja Mtume wetu Muhammad (saw), ada hii imepokelewa vizuri na waumini mbali mbali huku wengine wakiona kwamba ni jambo ambalo inabidi liwe ni mfano katika jamii nyengine, kwani wakinamama nao wakiachiwa waendeshe shughuli kama hizi wanao uwezo wa kuzifanikisha kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Katika hafla hiyo ambayo ilikusanya wageni kutoka mikoa mbali mbali nchini Tanzania, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini (TIC), ambae pia ni kaimu mkugenzi mkuu wa Hawza ya Im'am Sw'adiq (as) Sheikh Muhammad Abdu, alikuwa ndio mgeni rasmi, Sheikh Muhammad naye pia alipata nafasi ya kuongea na jamii hiyo ya kinamama hao wafuasi wa Ahlulbayt (as) na kutoa nasaha ambazo zilikuwa ni zenye manufaa kwa umma wa Kiislamu kwa ujumla.

Wanazuoni wametofautiana katika tarhe sahihi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw) ambapo kauli mashuhuri kwa wanazuoni wa Ahlu-Sunna inaashiria kwamba Mtume huyo (saw) alizaliwa mwezi 12 mfungo sita, huku wanazuoni wengi ambao ni wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt (as) wao wakiamini kwamba Mtukufu huyo wa daraja alizaliwa tareh 17 mfungo sita huo huo, kutokana na tofauti hiyo ya kauli hizo, wanazuoni wa madhehebu ya Shia ithnaasharia, wao wanaitambua wiki hii nzima ambayo ndani yake husemekana inasadifu kuzaliwa kwa mtukufu huyu wa daraja kama wiki ya umoja.

Baadhi ya picha za wakina mama walioshiriki katika zoezi hili ni kama ifuatavyo:

Maulidi ya kinamama yafanyika nchini Tanzania

Maulidi ya kinamama yafanyika nchini Tanzania

Maulidi ya kinamama yafanyika nchini Tanzania

Maulidi ya kinamama yafanyika nchini Tanzania

Maulidi ya kinamama yafanyika nchini Tanzania

Maulidi ya kinamama yafanyika nchini Tanzania

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha